<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Huyo ndiye! Anashuka TZR98</title>
<lyrics>[V1]
 Huyo ndiye! Anashuka
 Huyo ndiye! anaskuka,
 Aliyetufilia,
 Wengi waliookoka,
 Wakimfurahia,
 Aleluya!
 Yesu aturudia.

[V2]
 Sote tutamtazama,
 Amekaa kitini,
 Nao waliomcoma,
 Kumkaza mtini,
 Na kilio, wamuone enzini.

[V3]
 Alama za kifo chake
 Hata sasa anazo
 Na waaminifu wake
 Wapendezewa nazo.
 Alipata,
 Kwetu alama hizo.

[V4]
 Wokovu utakiwao
 Sasa wapatikana,
 Na watakatifu hao
 Mbinguni wakutana
 Kumlaki,
 Ndiyo siku ya Bwana

[V5]
 Wakusujudie wote
 Mbele ya kiti chako.
 Zako, Bwana, nguvu zote
 Itwae milki yako
 Njoo Bwana,
 Sisi tu watu wako.</lyrics>
<hymn_number>98</hymn_number>
</song>